Savio imeonyesha ukubwa wake katika Ligi ya Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BDL), baada ya kuifunga Mchenga Star kwa pointi 82-77 katika mchezo uliofanyika juzi usiku kwenye Uwanja wa Donbosco Osterbay.
Mchezo huo ulishuhudiwa na mashabiki wengi wakitaka kujua nani angeibuka na mshindi siku hiyo.
Akizungumza na Mwanaspoti baada ya mchezo kumalizika, kocha mkuu wa Mchenga Star, Mohamedi Yusuph alisema ulikuwa ni mzuri, lakini mipango yao ilishindwa kufua dafu mbele ya wapinzani wao.
“Kufungwa kwa timu yangu ni moja ya mchezo. Kwa kweli vijana wangu walipambana na sasa tunajipanga katika michezo inayofuata,” alisema Yusuph.
Akizungumza kuelekea kutafuta nafasi ya kucheza hatua ya nane bora, kocha huyo alisema licha ya ligi ya mwaka huu kuwa ngumu, anaamini timu yake itapambana ili kuhakikisha inacheza hatua hiyo.