Geita kasi ya ukuaji watu ni 5.4%

Imeelezwa kuwa Mkoa wa Geita watu wanakua kwa kasi kubwa kuliko ule wastani wa kawaida wa kitaifa ambapo takwimu zinaonyesha Mkoa wa Geita unakuwa kwa Asilimia 5.4 ambapo Kitaifa ni Asilimia 3.2.

Hayo yameelezwa na Mchambuzi wa Idadi ya watu na Maendeleo kutoka shirika la Kimataifa UNFPA Ramadhani Hangwa wakati alipokuwa akiwasilisha Taarifa fupi Mkoani Geita katika kuelekea kilele cha siku ya Idadi ya watu Duniani ambapo Kitaifa maadhimisho hayo yatafanyikia Mkoani Geita July 11 hapo kesho.

” Kama Kauri mbiu inasema tukija kutazama mkoa wa Geita una watu Milioni 2.9 ambapo kitaifa ni milioni 61 lakini ukiangalia kasi ya ukuaji watu kitaifa ni asilimia 3.2 lakini kwa mkoa wa Geita ni Asilimia 5.4 kwahiyo Mkoa wa Geita watu wanakua kwa kasi kubwa kuliko wastani wa kitaifa wa asilimia 3.2 kwa maana wao wanakuwa kwa asilimia 5.4 , ” Mchambuzi wa Idadi ya Watu na Maendeleo Hangwa.

 

Mchambuzi Hangwa amesema kwa wastani wa watoto kasi ya ukuaji kwa mkoa wa Geita wastani wake ni watoto sita huku akisema kwa takwimu za kitaifa zinaonyesha kwamba asilimia 11. 2 ya watu kati ya wale milioni 61 wana aina moja au zaidi ya ulemavu huku Mkoa wa Geita ukiwa ni asilimia 10.2.

Kwa upande wake Umrat Mohamed ambaye ni Afisa Mipango kutoka Tume ya Mipango Zanzibar amesema Mgeni rasmi katika Maadhimisho hayo Naibu waziri wizara ya Mipango na Uwekezaji Ndg. Stanslaus Nyongo huku akisema tayari Baadhi ya Vijana kutoka katika Mkoa wa Geita wameshiriki katika Makongamano ambapo mada mbalimbali ziliwasilishwa ikiwemo ushiriki wa Vijana katika Dira ya Taifa ya 2020 -2025.

” Tulianza na Makongamano ya Vijana ambapo vijana walitoka katika sehemu mbalimbali za Mkoa wa Geita walishiriki katika makongamano hayo ambapo mada mbalimbali zilizungumzwa ikiwemo ushiriki wa vijana katika Dira ya Taifa ya 2020- 2025 vijana walieleweshwa kwa namna ya kutoa maoni yao katika hiyo dita , ” Afisa Mipango Tume ya Mipango Zanzibar Bi. Umrat Mohamed.

Related Posts