Serikali yatenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa Daraja la Lumecha

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jenista Mhagama (Mb) Peramiho ameelekeza Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini (TARURA) Halmashauri ya wilaya ya Songea kuhakikisha daraja la Lumecha linajengwa ndani ya kipindi kifupi na kwa ubora.

Waziri ametoa kauli hiyoJulai 10,2024 wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi ya maendeleo katika kijiji cha Liweta Halmashauri ya wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.

“Serikali imetoa Sh milioni Nne kujenga madaraja na akiba ya fedha itakayobaki itatumika kutengeneza barabara mpaka kijiji cha Liweta ikiwa ni pamoja na kufukia shimo lilopo katika barabara hiyo alisema,” Waziri Mhagama.

Kazi ya ujenzi wa barabara ni muhimu naomba wananchi msaidie katika kulinda mradi ili ujenzi ili ukamilike kwa wakati na tufungue njia zitakazochochea uchumia katika kijiji cha Liweta.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jenista Mhagama (Mb) Peramiho amekagua ujenzi wa Godauni linaoendelea kujengwa ambalo litatumika kama soko la mazao katika kijiji cha Mpandangindo wakati wa ziara yake katika kata ya Mapandangindo.

Related Posts