Tchakei kulamba dili jipya Singida

UONGOZI wa Singida Black Stars (zamani Ihefu), umeanza mazungumzo ya kumwongezea mkataba mpya kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Marouf Tchakei.

Raia huyo wa Togo aliyejiunga na kikosi hicho Januari mwaka huu akitokea Singinda Fountain Gate aliyojiunga nayo kutokea AS Vita ya Congo, amekuwa na kiwango bora na msimu uliopita alifunga mabao tisa ya Ligi Kuu Bara na kuzivutia timu kadhaa.

Msimu uliopita wa Ligi Kuu Bara Tchakei, alicheza kwa ubora wa juu na kufunga mabao tisa na kutoa asisti tatu.

Kiwango alichoonyesha msimu uliopita kilimfanya kuanza kuhusishwa na klabu kubwa za Kariakoo, lakini dirisha la usajili lilipofunguliwa klabu hizo zimeonekana zikishusha vyuma bila ya kumtaja Tchakei. 

TIMU ya Dodoma Jiji iko katika mazungumzo ya kupata saini ya beki wa kati Mkongomani, Heritier Lulihoshi kutokea Tabora United.

Nyota huyo aliyewahi kucheza timu mbalimbali ikiwamo, Musanze FC ya Rwanda, inaelezwa hayupo tayari kubakia ndani ya kikosi hicho kwa msimu ujao hivyo ameanza mazungumzo na viongozi wake asepe.

KLABU ya Namungo imeanza mazungumzo ya kupata saini ya aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa kikosi cha Geita Gold, Geofrey Julius ‘Jojo’.

Jojo amemaliza mkataba na Geita itakayocheza Ligi ya Championship msimu ujao hivyo ameamua kutafuta changamoto mpya, huku Namungo wakiwa mstari wa mbele kumpata ili akakitumikie kikosi hicho cha Southen Killers.

Related Posts