Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Kituo cha kupokea, kupoza na kusambaza umeme wa Gridi ya Taifa kilichopo Inyonga Mkoani Katavi tarehe 13 Julai, 2024. Mhe. Rais Dkt. Samia anaendelea na Ziara yake ya Kikazi Mkoani humo ambapo atakagua na kufungua miradi mbalimbali ya Maendeleo pamoja na kuzungumza na Wananchi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Mlele katika muendelezo wa Ziara yake ya Kikazi Mkoani Katavi tarehe 13 Julai, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiondoka katika Kituo cha kupokea, kupoza na kusambaza umeme wa Gridi ya Taifa kilichopo Inyonga Mkoani Katavi mara baada ya kukikagua tarehe 13 Julai, 2024. Mhe. Rais Dkt. Samia anaendelea na Ziara yake ya Kikazi Mkoani humo ambapo atakagua na kufungua miradi mbalimbali ya Maendeleo pamoja na kuzungumza na Wananchi.
Sehemu ya Wananchi wa Mlele waliohudhuria Mkutano wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Wilayani hapo tarehe 13 Julai, 2024.
Shamrashamra za Wananchi wa Mlele wakati wa mapokezi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan mara baada ya kuwasili Wilayani hapo katika muendelezo wa Ziara yake ya Kikazi Mkoani Katavi tarehe 13 Julai, 2024.