Mabingwa wa michezo ya kubashiri kampuni ya Meridianbet leo imefunga safari kuelekea Kawe jijini Dar-es-salaam kwenye Zahanati inayopatikana sehemu hiyo na kufanikiwa kutoa msaada katika Zahanati hiyo.
Meridianbet imekua ikijitahidi kuhakikisha wanaigusa jamii inayowazunguka mara kwa mara haswa wale wenye uhitaji, Hivo leo sehemu yenye uhitaji leo imekua ni Zahanati hiyo inayopatikana katika eneo la Kawe.
Mabingwa hao wa michezo ya kubashiri wamefanikiwa kutoa mashuka zaidi ya 70 kwenye Zahanati hiyo, Mashuka ambayo yatatumika kwenye vitanda vya Zahanati hiyo ambapo yatakua msaada mkubwa kwani mashuka ni moja ya vifaa muhimu mahospitalini.
Bashiri mchezo wa Fainali ya michuano ya Euro 2024 unaotarajiwa kupigwa kesho kati ya timu ya taifa ya Hispania dhidi ya Uingereza ambao umepewa ODDS BOMBA sana. Bashiri sasa.
Kaimu wa kitengo cha Mawasiliano na masoko kutoka kampuni ya Meridianbet bwana Abubakar Kulindwa alikua muwakilishi wa taasisi alipata nafasi ya kuzungumza wakati wa ugawaji wa mashuka “Nipende kuwashukuru uongozi wa Zahanati hii kwa kutopokea mahali hapa lakini kubwa kutupatia ushirikiano katika kuhakikisha tunakamilisha jambo letu tulilolikusudia”
Shukrani hazikuishia hapo tu kwani Mwenyekiti wa eneo hilo anayefahamika kama Bi Aisha nae alipata wasaa wa kushukuru kutokana na kile kilichofanywa na Meridianbet, Huku akitoa wito kwa makampuni mengine kuiga mfano mzuri kwa mabingwa hao wa michezo ya kubashiri.