DC KIBAHA ATOA MAELEKEZO KWA WADAU WA MAJI KUHUSU UTUNZAJI WA MIUNDOMBINU YA MAJI

Mkuu wa wilaya ya Kibaha Mhe. Nickson Simon ametoa maelekezo kwa wadau wa maji kuhakikisha wanasimamia utunzaji wa miundombinu ya maji ambayo imejengwa na Serikali kuondoa Changamoto ya upatikanaji wa maji.

Saimon amesema kwa asilimia kubwa Serikali imeshakamilisha ujenzi wa miundombinu ya maji hivyo jukumu lililobaki ni wananchi kutunza na kuilinda miundombinu hiyo isiharibike.

Mkuu huyo wa Wilaya ametoa maelekezo hayo jana Julai 12 alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa mwaka wa wadau wa sekta ya maji ulioandaliwa na Mamlaka ya maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Kibaha

Saimon amemshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyopambana kuidhinisha fedha kwa ajili ya miradi ya maji.

Amesema mwaka 2023/2024 RUWASA Kibaha ilitengewa bilioni 1.7 na kwa mwaka huu wa fedha 2024/2025 wametengewa bilioni 3 na yote hayo ni kutimiza lengo la kumtua mama ndio kichwanj.

Akiwasilisha taarifa ya utendaji kazi wa Mamlaka hiyo Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kibaha Mhandisi Debora Kanyika amesema kwa mwaka wa fedha 2023/ 2024 walitengewa bajeti ya tsh 1.7 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji Kwala, Ruvu station, Miyombo ufugaji.

Miradi mingine ni Kigoda na upanuzi wa mradi wa Kimara Misale kwenda kigogo , Madege na Dutumi , Mradi wa kitongoji cha Masaki, na ukarabati wa Kipangege na mradi wa maji Dutumi.

Aidha Mhandisi Kanyika amesema kwa mwaka wa fedha 2023/2024 RUWASA imefanikiwa kukamilisha mradi wa maji Kwala, Mwembe Ngozi na Ruvu station.
Pia wameweza kufikisha huduma ya maji bandari kavu Kwala, kongani ya viwanda Sinotan, Kwala Marshaling yard , Ruvu station na TPS2 ambazo ni vituo vya reli ya mwendokasi ( SGR).

Kwa mujibu wa Mhandisi Kanyika kwa sasa idadi wananchi wanaopata huduma ya maji imeongezeka kutoka asilimia 67 hadi 78.

Mbunge wa viti maalum Hawa Mchafu ameipongeza RUWASA Kibaha kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kupeleka huduma kwa wananchi mafanikio yanaonekana tofauti na ilivyokuwa awali .

Pamoja na pongezi hizo Mchafu amewataka watendajiwa Mamlaka hiyo kuongeza bidii ya kazi na kukamilisha asilimia zilizobaki ili wananchi wote wa Kibaha wapate maji karibu na maeneo yao.

Rukia Bakari mkazi wa Ruvu Stesheni awali walikuwa wanakumbana na Changamoto ya maradhi ya kipindupindu kutokana na kukosa maji salama lakini sasa maisha yamebadilika baada ya kuunganishiwa maji ya bomba kwenye maeneo yao.

 

Related Posts