WATAHINIWA 22 WAFUTIWA MATOKEO FORM SIX – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) leo July 13,2024 limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha sita uliofanyika May mwaka huu 2024 ambapo pamoja na mambo mengine limefuta matokeo yote ya Watahiniwa 22 (17 wa Shule na 5 wa Kujitegemea) ambao walibainika kufanya udanganyifu katika Mtihani.

 

Akitangaza matokeo hayo leo July 13,2024 Visiwani Zanzibar, Katibu Mtendaji wa NECTA, Dr. Said Mohamed, amesema “Matokeo hayo yamefutwa kwa mujibu wa Kifungu cha 5 (2) (i) na (j) cha sheria ya Baraza la Mitihani sura ya 107 kikisomwa pamoja na Kifungu cha 30(2) (b) cha Kanuni za Mitihani Mwaka 2016”

Related Posts