Manchester United wanataka kumuuza mlinzi wa Uswidi Victor Lindelof, 29, msimu huu wa joto na pia watasikiliza ofa kwa ajili ya kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen, 32. (Manchester Evening News)
Chelsea wako tayari kumenyana na Tottenham, Bayern Munich na Paris St-Germain kumnunua kiungo wa kati wa Rennes Mfaransa Desire Doue, 19. (L’Equipe)
Manchester United wanavutiwa na mshambuliaji wa Brentford na England Ivan Toney, 28, ambaye yuko tayari kuhamia Old Trafford. (Christian Falk via Mail)
Klabu ya Serie A ya Como iko tayari kumsajili mlinzi wa Ufaransa Raphael Varane, 31, kama mchezaji huru baada ya kuondoka kwake Manchester United msimu huu. (Fabrizio Romano)
West Ham wameonesha nia ya kutaka kumnunua winga wa Uholanzi Steven Bergwijn, 26, lakini Marseille na vilabu viwili vya Saudi Arabia pia vinatumai kumnasa kutoka Ajax. (De Telegraaf)
Atletico Madrid wanatarajiwa kuipa AC Milan idhini ya kumsajili Alvaro Morata, 31, wiki ijayo baada ya kukamilisha majukumu yake ya kimataifa na Uhispania kwenye Euro 2024. (Calciomercato)
Everton, West Ham na Newcastle wanatazamiwa kumkosa Federico Gatti, 26, huku mlinzi huyo wa Italia akiwa tayari kuweka hatima yake kwa Juventus. (Tuttosport)
Mlinzi wa Ureno Nuno Tavares, 24, yuko mbioni kujiunga na Lazio kwa mkopo kutoka Arsenal. (Fabrizio Romano)
Winga Mfaransa Allan Saint-Maximin, 27, anatarajiwa kuondoka Al-Ahli ili kuungana na Jose Mourinho huko Fenerbahce. (Yagız Sabuncuoglu)
Arsenal, Manchester United na Aston Villa wanamuwania winga wa Girona na Ukraine Viktor Tsygankov, 26. (AS )
Nottingham Forest wameanza mazungumzo na Fiorentina kwa ajili ya kumnunua beki wa Serbia Nikola Milenkovic, 26. (Gianluca di Marzio)
Leicester wako tayari kutoa £21.5m kwa mshambuliaji wa Juventus Muajentina Matias Soule, 21. (La Gazzetta dello Sport )