VITUO VYA AFYA RUVUMA VYAPEWA MIEZI 5 KUKAMILISHA MFUMO WA GoTHoMIS

NA OR-TAMISEMI.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Bi. Rehema Madenge ametoa muda wa miezi mitano kwa vituo vya kutolea huduma za Afya katıka mkoa huo kukamilisha kufunga mfumo wa udhibiti wa taarifa za mgonjwa na mapato (GoTHoMIS) ili kuongeza kasi ya makusanyo na kutoa huduma bora kwa wananchi.

Bi. Madenge ametoa maelekezo hayo wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara ya timu ya Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe kutoka Ofisi ya Rais- TAMISEMI,Timu za Usimamizi wa Shughuli za Afya za Halmashauri(CHMT) na mkoa (RHMT) baada ya kukamilisha usimamizi shirikishi na ufuatiliaji wa huduma za Afya katika mkoa wa Ruvuma.

“Suala la kujiunga kwenye mfumo huu ni la muda mrefu sana na kutojiunga kwenye hii mifumo inaashiria kitu ambacho sio kizuri na tafsiri ya haraka na nyepesi maana yake kuna mambo ambayo tunayafanya na hatutaki kuyakosa na tukianza kutumia huu mfumo haya mambo tutayakosa ni lazima tuwe na ‘deadline’ na ‘deadline’ ambayo tumepewa ni kufikia mwezi disemba mwaka huu ‘fercilities’ zetu zote katika mkoa wa Ruvuma ziwe zinatumia ‘Centralised GoTHoMIS” amesema

Kwa upande wake mkurugenzi wa Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais – TAMISEMI Dkt. Rashid Mfaume amekemea matumizi ya fedha mbichi unaofanywa na uongozi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mbinga huku akisikitishwa na baadhi ya malipo katika Hospitali hiyo kufanyika kwenye namba ya simu ya mtu binafsi.

“Watu wanaidhinisha fedha mbichi ‘Cash’ ambayo imekusanywa na haijapelekwa benki kwasababu MOI (Mganga mfawidhi) ameagiza hiyo muisimamie CHMT Mbinga ile muikomeshe na mtengeneze kamati mkawahoji mambo yanayoendelea pale sio mbaya zaidi ‘Medical Officer Incharge’ ametoa namba yake binafsi akatoa kwa wateja” amesema Dkt. Mfaume

Timu ya Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe kutoka Ofisi ya Rais – TAMISEMI ikiongozwa na Dkt. Rashid Mfaume imekamilisha ziara yake katika mkoa wa Ruvuma na imeelekea katika mikoa ya Lindi na Mtwara kwaajili ya Usimamizi shirikishi na saidizi katika mikoa hiyo.

Related Posts