WAZAWA WAENDELEA KUITIKIA WITO WA SERIKALI KATIKA UWEKEZAJI NCHINI.

Wakazi wa Jiji la Dar es salaam na nje ya jiji hilo, wamepewa wito wa kuwekeza nchini kwani Serikali ya awamu ya sita imeweka mazingira rafiki, na kwa kufanya hivyo kutachochea maendeleo ya mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Wito huo umetolewa na Afisa Tarafa Ukonga, Kheri William, alipokuwa mgeni rasmi akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya Ilala, Edward Mpogolo, wakati akifungua L21 Executive Hotel ya mwekezaji Mzawa iliyoko Kata ya Kitunda, Jijini Dar-es-salaam iliyogarimu zaidi ya shilingi million 300 iliyo mita chache tu kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jiiini Dar es salaam.

Katika ufunguzi huo, William amesema “Uwekezaji huu utaongeza ajira, kuchochea ukuaji wa uchumi na kuongeza ukusanyaji wa Kodi mbalimbali za Serikali.

“Serikali ya Awamu ya sita chini ya Rais Dokta Samia Suluhu Hassan imeweka mazingira rafiki ya uwekezaji na ukusanyaji wa kodi rafiki isiyotumia nguvu”

Kwa upande wake, Meneja wa Hotel hiyo yenye vyumba 10, Hanns Maginus, amesema uwekezaji huo utachochea pia ukuaji wa uchumi kwa serikali na wakazi wa Kitunda kupita ajira mbalimbali zitakazopatikana.
Naye, Diwani wa Kata ya Kitunda, Victor Vedasto, ameupongeza uongozi wa Hoteli ya L21 Executive kwani kwa uwezekezaji huo wametengeneza fursa za ajira na kuongeza ukusanyaji wa Kodi za serikali.

 

Related Posts