UDSM NA CHUO KIKUU CHA ZHEJIANG CHINA KUSHIRIKIANA UBORESHAJI MASOMO YA SAYANSI

CHUO Kikuu Cha Dar es Salaam kwa kushirikiana Chuo kikuu Cha Zhejiang kutoka China wamefungua Mkutano wa Pili unawakutanisha wataalamu wa elimu kada ya sayansi kwa lengo la kuwasaidia wataalamu hao kutambua namna bora ya ufundishaji wa masomo ya sayansi.

Hayo  yamebainishwa na Mkurugenzi wa Elimu ya Juu,Bw.Peter Makenga wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari  jana 11,2024 katika Ukumbi wa UDSM  Jijini Dar es Salaam.

Aidha Makenga ameeleza kuwa nchi ipo katika maboresho makubwa ya mtaala wa elimu ambao unasisitiza elimu ya sayansi, suala la Hisabati, utafiti pamoja na ubunifu.

“Ukiangalia kwa makini mtaala wetu mpya unamtaka Mwanafunzi au yule anaejifunza aweze kupambana na yyanayotokea sasa au yaale yajayo,maana yake ni kwamba tunamtengeneza tunamtengeneza Mwanafunzi atakayetumika hapa Tanzania aau katika dunia”ameeleza.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Prof. William Anangisye amesema kuwa mkutano huo umefanyika kutokana na matokeo ya tafiti zilizofanywa ambapo watafiti nchini watapata wasaa wa kueleza matokeo ya tafiti zao jinsi zinavyoweza kuisaidia jamii.

Naye Mwakilishi kutoka Chuo Kikuu Cha Zhejiang amesema urafiki kati ya China na Tanzania unatoa nafasi ya kubadilishana walimu wa masomo ya sayansi ambapo yataleta tija kwa maendeleo ya dijitali na kuchagiza ongezeko la wasomi wa kidijitali.










Related Posts