FCC YAJIVUNIA MAFANIKO WALIYOYAPATA MAONESHO YA 48 YA SABASABA 2024

 

Na Emmanuel Massaka,Michuzi TV

Tume ya Ushindani (FCC) imetoa elimu na semina kwa wafanyabiashara na wajasiliamali zaidi  2000 katika Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara yajulikanayo kama Sabasaba. 

Elimu tuliyoitoa kwa wananchi waliotembelea banda letu ni Masuala la Ushindani, Kumlimda Mlaji na Mtumiaji na kuwapa elimu ya kuzitambua bidhaa bandia. 

Akitoa taarifa hiyo leo ikiwa ni siku ya mwisho ya Maonesho hayo Julai 13, 2024

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma (FCC) Bi. Roberta Feruzi amesema wamemaliza kwa mafanikio makubwa sana maana wamewafikiwa kutoa elimu na mafunzo kwa makundi mbalimbali. 

“Sisi FCC mbali na kuwa na banda tulifanya kampeni ya banda kwa banda walipo wajasiriamali na tumefanikiwa kutoa elimu na semina kwa Wajasiriamali wanaosimamiwa na Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO), Umoja wa Wafanyabishara Wanawame. 

Amesema kuwa FCC kwa sasa wamezidi kuwafikia wateja wao kwa kufungua  ofisi za Kanda ili kuweza kusambaza elimu zaidi.

Amezitaja Kanda hizo, ikiwemo Kanda ya Ziwa inayohudumia mikoa Sita ofisi yake ikiwa mkoani Mwanza, Nyanda za Juu Kusini inahudumia mikoa 5 na ofisi yake ikiwa mkoani Mbeya na Kanda ya Kaskazini inahudumia mikoa 5 ofisi ikiwa mkoani Arusha. 

Bi. Feruz ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutembelea ofisi za FCC na mitandao yao ya jambo ili waendelee kupata elimu zaidi juu ya bidhaa bandia na masuala mazima ya kuwalinda wazalishaji na walaji. 

Vile vile ameiomba jamii kuendelea kutoa taarifa za wazalishaji wa bidhaa bandia ili kuweza kukomesha tabia hizo. Mwisho alitoa shukrani wa Tantrade kwa kuendelea kuandaa maneno hayo yaliyoleta manufaa zaidi katika kukuza uchumi wa nchi. 

Kwa upande mmoja ya wananchi aliyetembelea banda la FCC Dr Kharid amewashukuru kwa kutoa elimu mbalimbali na kuwafanya watambue tofauti ya bidhaa bandia na zile halisi.

Kama inavyoonekana pichani  Maafisa wa Tume ya Ushindani (FCC) wakiendelea na kazi ya kuwahudumia wananchi.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MASSAKA, MICHUZI TV)

 

Related Posts