ISHU YA MANULA SIMBA IPO HIVI – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Crescentius Magori amefunguka Kuhusu ishu ya kipa Aishi Manula ambaye yupo nje ya kambi ya timu, alisema ni mchezaji wao hadi hapo taarifa nyingine itakapotolewa.

 

“Manula bado ni mchezaji wa Simba na siwezi kulizungumzia hili sana, kwa sababu halipo chini yangu labda mtendaji mkuu wa klabu ndio anaweza kulieleza kwa usahihi na jana alikutana na mchezaji huyo,” alisema.

 

 

“Ila ninachofahamu ni mchezaji wa Simba kama kutakuwa na mabadiliko ufafanuzi utatolewa na kuhusiana na mshambuliaji wetu Aubin Kramo pia bado tuna mazungumzo naye juu ya kumtoa kwa mkopo au kumalizana naye kabisa.”

 

[via Azam TV]

 

Related Posts