MADINI NI MAISHA NA UTAJIRI – MWANAHARAKATI MZALENDO

Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limetoa elimu kwa Umma namna litekeleza Vision 2030 Madini ni Maisha na Utajiri yenye lengo la kufanya utafiti wa madini wa kina kwa asilimia 50 ya nchi nzima ifikapo mwaka 2030.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO , Dkt. Venance Mwasse wakati ametembelea Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba Jijini Dar es salaam yaliyoanza Juni 28 na kumalizika Julai 13, 2024.

Mwasse ameongeza kuwa katika kutekeleza mkakati wa Vision 2030, STAMICO inaendelea kuboresha miradi yake ukiwemo mradi wa uchorongaji, uchimbaji wa madini ya dhahabu na makaa ya mawe, uzalishaji wa nishati mbadala ya Rafiki Briquettes pamoja na kuboresha mazingira bora kwa wachimbaji mdogo.

Akielezea kuhusu Sekta ya madini kufungamanishwa na sekta nyingine za kiuchumi , Dkt.Mwasse ameeleza kuwa kwa kuangalia umuhimu wa Nishati safi , STAMICO imeamua kuzalisha nishati mbadala ya kupikia ya Rafiki Briquettes iliyotokana na kuongezea thamani mabaki ya makaa ya mawe kwa lengo la kubeba ajenda ya utunzaji mazingira .

Naye ,Bi. Bibiana Ndumbaro Afisa Uhusiano kutoka STAMICO ameongeza kuwa Shirika linaendelea kutoa ajira kupitia miradi yake ikiwemo uchorongaji, uzalishaji wa mkaa mbadala ambapo mpaka sasa zaidi ya vijana wa kitanzania wanashiriki katika kutekeleza miradi hiyo.

Ndumbaro amefafanua kuwa STAMICO inaendelea kutanua wigo wa uchimbaji madini wenye uhakika kwa kusaidia kufanya utafiti wa kina katika mashapo ili kupata taarifa sahihi za kiwango cha madini kilichomo katika maeneo hayo ya uchimbaji hivyo kupunguza athari za kiuchumi kwa wachimbaji zinazotokana na uchimbaji wa kubahatisha. Vision2030: Madini ni Maisha na Utajiri

Cc:W/Madini

#KonceptTvUpdates

Image

Related Posts