MADRID WAUZA TIKETI ZOTE UTAMBULISHO WA MBAPPE BERNABEU – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

Klabu la Real Madrid ya nchini Hispania, imetangaza kuuzwa kwa tiketi zote kwa ajili ya mapokezi ya nyota wa timu ya Taifa ya soka ya Ufaransa, Kylian Mbappé aliyejiunga na klabu hiyo.

Mapokezi ya Mbappé yatafanyika siku ya Jumanne katika Uwanja wa Santiago Bernabeu, ambapo zaidi ya mashabiki 85,000 watakuwepo uwanjani hapo.

Habari zaidi zinaeleza kuwa, baadhi ya tiketi zimelazimika kuuzwa kwa bei ghali kutokana na uhitaji, ambapo idadi kubwa ya watu walizihitaji ili waweze kuingia uwanjani.

Siku hiyo muhimu ya mapokezi yake, Mbappé atakuwepo pamoja na familia yake, ambapo kwa upande wa Real Madrid wamealika baadhi ya magwiji wa klabu hiyo kumkaribisha.

Ndani ya Real Madrid, Mbappe atavaa jezi namba 9.

Kabla ya kujiunga na Real Madrid, Mbappe alikuwa akiichezea klabu ya Paris Saint-Germain (PSG) ya nchini Ufaransa.

Related Posts