MSHAMBULIAJI mzawa aliyemaliza na mabao 12 katika Ligi Kuu Bara msimu uliopita, Wazir Junior Shentembo yupo katika mazungumzo ya kutaka kurejea tena Dodoma Jiji akitokea KMC.
Inadaiwa mabosi wa Dodoma wapo hatua za mwisho za kukamilisha dili hilo la nyota huyo wa zamani wa Toto Africans, Yanga na Mbao FC.
Awali, nyota huyo alikuwa akipigiwa hesabu na klabu za Singida Black Stars na Pamba Jiji zilizoonyesha nia ya kumhitaji, kabla ya Dodoma Jiji kuingilia kati na muda wowote huenda jamaa akaibukia kwenye timu hiyo aliyowahi kuitumikia kabla ya kutua KMC.
Wazir amekuwa na msimu mzuri uliopita wa Ligi Kuu Bara akiwa ndiye mshambuliaji aliyefunga mabao mengi zaidi katika ligi nzima katika msimu ambao ulitawaliwa na viungo, Stephane Aziz Ki wa Yanga akimaliza mfungaji bora kwa kufunga mabao 21, akifuatiwa na Feisal Salum ‘Fei Toto’ wa Azam (mabao 20). Kisha wa tatu akawa Wazir Jr, akiwa mshambuliaji pekee kwenye Top 3.
Mahali: Nyamagana, Mwanza
Alikopita: Toto Africans, Azam FC, Biashara Unitd, Mbao, Yanga, Dodoma Jiji