TANGA UWASA KUNUFAIKANA NA MRADI WA “GREEN SMART CITY SASA” – MWANAHARAKATI MZALENDO

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga UWASA) kwa kushirikiana na uwakilishi kutoka Dutch Water Operator (VEi), wamesaini mkataba wa kuanza rasmi kwa utekelezaji wa mradi wa “Usalama wa Maji na uimara wa hali ya hewa kwa maeneo ya mijini nchini Tanzania (Green and smart city sasa Project).

Mradi huu umelenga kuimarisha utendaji wa Tanga UWASA katika nyanja za uzalishaji na usambazaji maji, huduma kwa wateja na udhibiti wa maji yanayopotea (Non- revenue water), ambapo kazi zitakazotekelezwa zitahusisha;

1. Utengenezaji na ufungaji wa Water district metered areas (DMAs).

2. ⁠Uboreshaji wa mfumo wa GIS

3. ⁠Uboreshaji wa mfumo wa utoaji wa taarifa za mivujo na njia za haraka za kufikia mivujo na kuidhibiti.

4. ⁠Kutoa mafunzo ya upimaji, usomaji na ufungaji wa mita za maji.

5. ⁠Kuboresha huduma za Usafi wa mazingira mashuleni.

6. ⁠Kuendeleza mtandao wa majisafi na kuunganisha wateja kwa Kaya zisizo na uwezo.

Mradi huu unatekelezwa kwa kipindi cha miaka miwili (2) kuanzia Julai, 2024 hadi Oktoba, 2026 ambapo gharama yake ni Shilingi za Kitanzania 2,900,437,900.

#KonceptTvUpdates

Inaweza kuwa picha ya Watu 9

Related Posts