ARGENTINA BINGWA COPA AMERICA 2024 – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

Timu ya taifa ya Argentina imetwaa ubingwa wa kombe la Mataifa Amerika Kusini, Copa America 2024 kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Colombia kwenye fainali iliyopigwa katika dimba la Hard Rock, Miami asubuhi hii.

Lautaro Martinez amefunga bao lake la 5 kwenye michuano hiyo na kuisaidia Argentina kutwaa Copa America kwa mara ya 16 na kuipiku Uruguay kama timu yenye makombe mengi zaidi ya Copa America. Uruguay imetwaa mara 15 huku Brazil ilitwaa mara 9.

Argentina sasa wametwaa kombe la nne mfululizo la michuano mikubwa ya kimataifa baada ya kutwaa Copa America 2021, Finalissima 2022, Kombe la Dunia 2022 na Copa America 2024.

Lautaro Martinez amemaliza kama mfungaji bora wa michuano hiyo akiwa na magoli matano huku kiungo wa Colombia, James Rodriguez akimaliza kinara wa pasi za mwisho (assists) akiwa na asisti 6 pamoja na kufunga bao moja.

 

Related Posts