Urusi kuifaidisha Tanzania na kukuza ushirikiano wa kibiashara

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni ,Sanaa na Michezo Gerson Msigwa amewaalika wawekezaji kutoka nchini russia wafanyabiashara na sekta binafsi ya Urusi kuja kuchangamkia fursa nyingi ambazo bado hazijatumika Tanzania ikiwemo gesi.

Akifungua mkutano baina ya wafanyabiashara wa Tanzania na Russia kwenye kongamano la kibiashara ambalo limepewa jina Russia Day(Siku ya Russia).
alisema kuna maeneo mengi ya kuwekeza nchini na kuwaalika wawekezaji kutoka nchi hiyo kuwekeza.

Alisema sekta za madini na gesi zinafursa nyingi za kuwekeza hivyo kuwaalika wake wawekeze na Serikali ipo tayari kushirikiana nao .

Alisema serikali imeamua kufanya hivyo ili kutengeneza jukwaa zuri zaidi la namna nchi hizo zinaweza kushirikiana katika biashara na uwekezaji.

“Bado nchi inahitaji uwekezaji mkubwa leo ni siku ya Urusi pamoja na hotuba zimetolewa na viongozi wafanyabiashara wanapata fursa ya kukutana kubadilishana mawazo,”alisema.

Alisema kwasababu nchi bado wanahitaji uwekezaji katika sekta mbalimbali ikiwemo kilimo,madini, biashara, utalii na maeneo mengine serikali imeweka utaratibu mzuri kupitia Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

Alisema kuwa muhimu ni teknolojia wamepiga hatua ni moja ya changamoto kubwa nchini waliyonayo teknolojia ndogo kutumia katika uzalishaji

Kwa upande wake Balozi wa Urusi nchini Tanzania, Andrew Avetisyan alisema kongamano hilo ni muhimu kwa wafanyabiashara wa nchi zote mbili kubadilishana uzoefu na fursa za uwekezaji.

Alisema Urusi na Tanzania wamekuwa na ushirikiano mzuri hivyo maenesho hayo watatumia kuonesha bidhaa mbalimbali za nchi hizo.

“Tupo tayari kusaidia wafanyabiashara wa Tanzania na kufanya uwekezaji nchini na kubadilishana uzoefu na ujuzi katika masuala mbalimbali,” amesema Avetisya

Avetisyan alisema kongamano hilo ni muhimu kwa wafanyabiashara wa nchi zote mbili kubadilishana uzoefu na fursa za uwekezaji.

Related Posts