Banda aisikilizia Richards Bay | Mwanaspoti

BEKI Abdi Banda licha ya timu aliyoichezea msimu ulioisha Richards Bay kumpa nafasi ya kuongeza mkataba wa mwaka mmoja baada ya kumalizika wa awali, bado akili yake inawaza kusaka changamoto mpya.

Katika mahojiano yake na Mwanaspoti, Banda alisema timu ya Richards Bay inasubiri uamuzi wake, lakini anajipa nafasi ya kuwaza zaidi changamoto mpya katika timu nyingine zinazohitaji huduma yake.

“Nashindwa kusema nitaendelea na Richards Bay ama nitaondoka, sababu kubwa mchezaji hadi akisaini katika timu anakuwa ameangalia vitu vingi, yakiwemo maslahi.

Aliongeza”Tanzania nipo kwa muda mfupi, kwani nilikuwa mapumziko, ingawa nilikuwa naendelea kujifua na mazoezi ndio maana umenikuta hapa Uwanja wa Bora, nikiwa nacheza, lengo langu nikujiweka fiti.”

Banda ambaye alijiunga na Richards Bay msimu uliopita akitokea Chippa United, aliizungumzia  Ligi ya Afrika Kusini, kwamba kwa sasa haina utofauti sana na Ligi Kuu Bara.

“Ligi yao ni nzuri, ingawa haijatofautiana sana na Tanzania ambako wachezaji wengi kutoka nje wanatamani kuja kucheza, walichotuzidi ni miundo mbinu wao wapo juu zaidi,” alisema.

Related Posts