Polisi nchini Kenya wamemkamata mwanaume mmoja anayefahamika kama Jomaisi Khalisia (33) ambaye wanadai amekiri kuwaua wanawake 42 tangu 2022, akiwemo mkewe .
Msako wa mtuhumiwa huyo ulianza baada ya mauaji ya kutisha ya wanawake tisa ambao miili yao iliyokatwakatwa ilipatikana kwenye machimbo ambayo yanatumika kama jalala.
Mshukiwa amekamatwa katika baa mapema Jumatatu asubuhi alipokuwa akitazama fainali ya Euro.
Polisi wamesema mtuhumiwa huyo amekiri kuwarubuni, kuwaua na kutupa miili ya wanawake 42 katika eneo hilo la taka .
Mohamed Amin ambaye ni mkuu idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) amesema wamepata ushahidi muhimu katika nyumba ya mtuhumiwa, zikiwemo simu 10, tarakilishi bebe , panga, vitambulisho na mavazi ya kike.