Rais Dkt. Samia ahitimisha ziara yake Mkoani Katavi kwa kuzungumza na Wananchi wa Mpimbwe

Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ahitimisha ziara yake Mkoani Katavi kwa kuzungumza na Wananchi wa Mpimbwe katika Jimbo la Kavuu mkoani humo.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Mpimbwe katika Jimbo la Kavuu mkoani Katavi tarehe 15 Julai, 2024. Mhe. Rais Samia amehitimisha Ziara yake mkoani Katavi na Kuendelea na Ziara yake Mkoani Rukwa kwa kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo na kuzungumza na Wananchi.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwasikiliza Wananchi wa Mpimbwe katika eneo la Kibaoni kabla ya kuhitimisha ziara yake Mkoani Katavi tarehe 15 Julai, 2024.

Wananchi wa Mpimbwe kwenye Jimbo la Kavuu mkoani Katavi wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika eneo la Kibaoni tarehe 15 Julai, 2024.

Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda pamoja na Wananchi wa Mpimbwe wakishangilia mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwasili katika eneo la Kibaoni wakati akihitimisha ziara yake Mkoani Katavi tarehe 15 Julai, 2024.

Related Posts