RAIS WA ZANZIBAR DKt. MWINYI AFUNGUA BUSTANI YA MNAZI MMOJA MJI MKONGWE JIJINI ZANZIBAR

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikata utepe kuifungua Bustani ya Mnazi Mmoja Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar, iliyoko jirani na Hospitali ya Mnazi Mmoja, ufunguzi huo uliyofanyika leo 15-7-2024, na (kulia kwa Rais) Mwenyekiti wa Kampuni ya Infinity Group Bw. Samuel Saba na ( kushoto kwa Rais) Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akitembelea bustani ya Mnazi Mmoja Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar, baada ya kuifungua leo 15-7-2024, akiwa na Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga.

BAADHI ya Wageni waalikwa katika ufunguzi wa Bustani ya Mnazi Mmoja Wilaya ya Mjini Unguja jirani na Hospitali ya Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi. (hayupo pichani) akizungumza na kuifungua bustani hiyo ufunguzi huo uliofanyika leo 15-7-2024.

AIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiondoa pizia kuweka Jiwe la Msingi la Ufunguzi wa Bustani ya Mnazi Mmoja (Jirani na Hospitali ya Mnazi Mmoja) Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar na Mwenyekiti wa Kamapuni ya Infinity Group Bw. Samuel Saba (kushoto) ufunguzi huo uliyofanyika leo 15-7-2024 na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said.

(Picha na Ikulu)

Related Posts