KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka Halmashauri zote Nchini kuhakikisha zinatekeleza miradi ya kimaendeleo kwa kufuata sheria na kuzingatia mfumo wa kidigitali wa manunuzi ya UMMA unaosimamiwa na PPRA unaolenga kudhibiti rushwa na kuongeza ushindani kwa kuwapata wazabuni wenye sifa katika utekelezaji wa miradi ya Serikali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Morogoro … (endelea).
Akitoa agizo hilo baada ya kukagua na kuzindua ujenzi wa Daraja la Kalavati la Masombawe linalounganisha kata za Mtumbatu, mamboya na Magubike Wilayani Kilosa ikiwa ni ishara ya kwenda kumaliza adha ya Wanafunzi waliokua wakipata changamoto za kuvuka Kwenda shuleni kutokana na kukosekana kivuko cha uhakika pamoja, kiongizo wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava ameipongeza Kilosa kufuata sheria na utaratibu wa utekelezaji wa miradi yake huku akizitaka Halmashauri zote Nchini kufuata utaratibu huo.
Kutokana na kufunguliwa kwa Daraja hilo la Kalava lenye midomo minne lililogharumu zaidi ya milioni 300, Mbunge wa Jimbo la Kilosa Prof. Palamagamba Kabudi akaishukuru Serikali kwa kuendelea kuifungua Wilaya ya Kilosa kutokana na utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM ambapo alimshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuleta fedha za Maendeleo.
Wilaya ya Kilosa umekimbiza Mwenge wa Uhuru kwa kupita katika miradi saba ya kimaendeleo yenye thamani zaidi ya shilingi bilioni 2.88 ambapo ulikimbizwa umbali wa km 331.9 katika Tarafa sita kati ya saba, kata 21 kati 40 na vijiji 37 kati ya 138 ambapo utapitia jumla ya miradi sita ya maendeleo na shule ya wanafunzi wenye mahitaji maalum.
Mwenge Uhuru katika Wilaya ya Kilosa ulizindua 4 itazinduliwa, Mradi mmoja kufunguliwa na miradi 2 kuonwa ambapo Miradi hiyo ipo katika Sekta ya Elimu, Afya, Barabara, Maji, Kilimo na Maendeleo ya Jamii. utakimbizwa ndani ya jamii.