Bunge jipya ya Ufaransa kukutana Alhamisi wiki hii – DW – 15.07.2024

15 Julai 2024

Wabunge kadhaa wa chama cha muungano wa mrengo wa kushoto nchini Ufaransa wamesema,kwamba chama hicho kinalenga kunyakuwa nafasi ya spika wa bunge wakati bunge hilo litakapofunguliwa kwa mara ya kwanza alhamisi wiki hii.

https://p.dw.com/p/4iJaq

Ufaransa  | Muungano wa vyama vya mrengo wa shoto
Muungano wa vyama vya mrengo wa shoto nchini Ufaransa.Picha: Frederick Florin/AFP/Getty Images

Chama hicho kimesema kinataka kupata nafasi hiyo ili kuwa na nguvu bungeni licha ya kutokuwa na wingi mkubwa wa viti na kinashindwa  kuunda serikali baada ya uchaguzi wa mapema wa bunge.

Wabunge watakuwa na jukumu Alhamisi la kumchaguwa spika,ambayo ni nafasi muhimu katika kipindi hiki ambacho rais Emmanuel Macron amedhoofika kisiasa na bunge likiwa na mgawanyiko kutoka na kutokuwepo chama au kundi lenye wingi wa kutosha wa kudhibiti mamlaka peke yake.

Related Posts