CEO SIMBA ANG’ATUKA – MWANAHARAKATI MZALENDO

Bodi ya Wakurugenzi ya klabu ya Simba imeridhia kuachana na Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa klabu hiyo Imani Kajula baada ya yeye mwenyewe kuomba kuondoka pindi mkataba wake utakapoisha.

 

Kupitia taarifa iliyotolewa na idara ya Habari na Mawasiliano ya klabu hiyo leo, Jumatatu Julai 15.2024 imeeleza kuwa Kajula ataondoka mwishoni mwa mwezi Agosti 2024 ikiwa ndiyo mwisho wa mkataba wake.

 

Kajula alianza kufanya kazi Simba January 26.2022 hata hivyo hakuwa na mafanikio makubwa kama ilivyotarajiwa.

 

Related Posts