Wanawake Watumishi na waliowahi kuwa Watumishi wa Wizara ya fedha ambao wanaunda umoja wa Golden Women Gala wametakiwa kutochukiana na kutokuwa sababu ya yeyote kutofanikiwa katika kazi na hasa katika upandaji wa vyeo na mambo mengine.
Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Jenipher Chirstian Omolo mapema Jijini Dodoma,katika sherehe za Wanawake Watumishi wa Wizara wakati akiwa mgeni rasmi ambapo amezindua rasmi umoja huo ulioshajihishwa na kauli mbiu isemayo:UMOJA WA WANAWAKE KATIKA AJIRA, NI HAZINA YA MAENDELEO.
“Furahia kuona wenzako wa chini wanapanda,usimchimbie mwenzako kaburi Mungu hapendi hakikisha unakuwa kiongozi ambaye unafurahia mema ya wengine sio kufanya ili faili la mtu halipandi kwani na kwa watoto wako halitapanda, ndo principle za Mungu kuwa ukimtendea mtu mabaya nao watoto wako watatendewa mabaya”.
Aidha Naibu Katibu Mkuu huyo ameongeza kwa kuwataka Wanawake wa Wizara hiyo kujiamini na kuonesha uwezo wa kazi wa hali ya juu wawapo katika Maeneo yao ya kazi kwani ndio utakao wainua na kuwapandisha juu na sio kutegemea upendeleo kutoka kwa mtu mwingine kwani huwa ni wa muda tu.
“Hata kama ofisi ina wanaume 6 na wewe mwanamke ukawa mmoja fanyakazi kwa uwezo wako kwani hakuna mtu ambaye hajui kazi,kwahiyo jiamini fanya kazi Mungu atakupandisha usitake kuoanda kwa upendeleo wa watu. Sasa kuna tabia tunakuwaganazo za kuataka kupanda kwa upendeleo wa watu hayo ni ya muda mfupi kwani atakupandisha leo kesho hayupo, pia unapokuja kazini ujue kilichokuleta ni kazi na mahusiano ya kawaida na watu wa pale kazini, ukionesha uwezo wako watakuheshimu na usiotengeneza kuheshimika watu watakudharau”.
Pia hakuacha kuwatia moyo wanawake kuwa wanapohisi kulemewa nakusongwa na mambo magumu katika majukumu yao na hata familia wamkombilie Mungu kwani ndiye miweza ya wote na baada ya hapo ndo waone kama wanaweza kwenda kwa wataalam wa Afya ama vinginevyo.
Awali akisoma Risara ya Umoja wa wanawake wa GWG Mwenyekiti wa umoja huo Consolatha Maimu amesema kuwa lengo kubwa la kuanzishwa kwa umoja huu ni kuwaleta pamoja wanawake ili kushirikiana katika masuala ya kijamii pamoja na kudumisha umoja,kufarijiana,kusaidiana katika shuda na raha na kutiana moyo.
Na kuongeza kuwa katika kuashimisha mwaka mmoja wa umoja huo mafunzo yametolewa kwa kina Mama kuhusu namna ya kukabiliana na changamoto wanazokutana nazo katika maeneo ya kazi.
“Lengo kubwa la kikundi ni kuwaleta pamoja Watumishi wanawake ili kushirikiana katika masuala ya kijamii pamoja kudumisha umoja,kufarijiana,kusaidiana katika shida na raha na kutiana moyo”.
“Katika kuashimisha mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa umoja huu umeandaa sherdhe hii ili kufanya Uzinduzi na mkuwa mwaka,kutoa mafunzo kwa kina Mama wote kuhusu namna ya kukabiliana na changamoto zinazowakabili katika maeneo ya kazi na ulezi wa familia ikiwa ni pamoja na wamama kufarahi kwa pamoja”.
Avemaria Lukanga ambaye ni….wakati akiwasilosha moja ya mada zilizotolewa katika kongamano hili amewaasa wanawake kujitokeza kujiunga na Hazina saccos kwani kuna mbalimbali lakini pia wameanzisha Mkopo wa Tuliza.moyo ambao humsaidia mwanamke na kumuepusha na mikopo ya kausha dam huko ambayo imekuwa na ni changamoto kwa wanawake wengi.
“Tuna mkopo wa Tuliza moyo,hu mkopo tuliupendekeza baada ya kuina watu wanateseka na huko mtaani na kausha damu tukaona kwanini wanachama wetuwakaushwe damu wakati tuna uwezo wa kuwatuliza moyo,kwahiyo tukawatuliza moyo kwa mkopo wa chap chap yaani ukileta fomu unapewa milioni moja ambayo utarejesha ndanj ya mwezi pasipo na changizo la riba yetote”.
Dkt Swai Japhet ambaye ni Mtaalam Bingwa wa Saikolojia na Afya ya akili kutoka Hospital ya Afya ya akili Milembe Dodoma ametumia nafasi hii kuwakumbusha Wanawake katika masuala ya malezi ya watoto kwani malezi hayo ndio yanayoamua mtoto kuwa na tabia atakazokuwa nazo,na kusema kuwa watoto wote huzaliwa ubongo ukiwa mweupe mfano wa karatasi hivyo hivyo matokeo ya mtoto ni mambo anayoyapata katika jamii.
Pia Dkt Swai ametoa mambo ya kusaidia kutunza afya ya akili ambapo amesema hata kulala vizuri kuanzia walau masaa 7 nayo pia ni kitu ambacho kinaweza kusaidia kutunza afya ya akili ya mtu.
“.na kwa wale wenye watoto hebu waanze kufikiria kuhusu watoto kwani mtoto anapozaliwa ubongo huwa mweupe mfano wa karatasi,hivyo matokeo na tabia za mtoto ni mambo anaykutana nayo kwa wazazi wote wawili na jamii kwa ujumla”.
Hili ni tukio la kwanza la Umoja wa kina wa Golden Women Gala ambao wameajiriwa Wizara fedha na kina Mama waliowahi kuwa Wizara ya fedha na sasa wamehamia sehemu mbalimbali lakini Makao makuu ni hapa Dodoma na ulianzishwa Tarehe 2 July 2023 ukiwa na wanachama 247 na wengine waliendelea kujiunga mpaka kufika wanachama 288.