REAL MADRID KUMTANGAZA RASMI KYLIAN MBAPPE LEO – MWANAHARAKATI MZALENDO

Na Mwandishi Wetu; Mabingwa watetezi wa Ligi kuu ya La liga (2023/24) Real Madrid leo wameandaa hafla ya kumtangaza rasmi nyota raia wa Ufaransa Kylian Mbappe kama mchezaji mpya wa klabu hiyo leo saa moja kamili usiku.

Real Madrid imemsajili Straika huyo hivi karibuni baada ya mkataba wake na klabu ya PSG kufikia kikomo msimu huu uliomalizika.

Imethibitishwa kuwa tickets 85,000 za mashabiki watakao shuhudia tukio hilo la leo zimeisha; na uwanja unatarajiwa kujaa ifikapo muda husika wa tukio.

Kylian Mbappe anatarajiwa kuvaa Jezi Namba (9) na sio (10) kama ilivyozoeleka kwa kuwa anaheshimu uwepo wa kiungo wa Real Madrid Luka Modric anayetumia Namba (10) sasa.

Kylian Mbappe ni kati ya nyota bora zaidi wa soka la kulipwa hivi sasa. Na ni kati ya wanasoka wanaolipwa hela nyingi zaidi duniani hivi Leo.

Imeandikwa na; Altman Milton

#KonceptTvUpdates

Related Posts