RAIS SAMIA AWATAKA WATANZANIA KUTUNZA BARABARA – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka Watanzania kutunza barabara zinazojengwa Nchini kwakuwa ujenzi wake unatumia gharama kubwa.

 

Rais Samia amesema hayo leo July 16,2024 wakati akizindua barabara ya Sumbawanga – Matai – Kasanga ikiwa ni sehemu ya ziara yake Mkoani Rukwa.

 

“Kwa upande wa barabara nizungumze na Wasafirishaji, kawaida magari yetu yakiharibika tunaegesha tu pembeni halafu tunasubiri matengenezo yaendelee, wakati tunaegesha magari mengine yanamwaga dizeli kwenye barabara na kusababisha barabara iharibike, iwe na matundu na mashimo na ndio mwanzo wa barabara kuharibika”

 

“Lingine Wananchi kufukuafukua, kulimalima na kuchimbachimba pembezoni mwa barabara kunasababisha mmomonyoko wa barabara, huu sio mtindo mzuri na maisha ya barabara yanakuwa mafupi sana, ujenzi wa barabara ni gharama sana, ukijenga KM 1 ya barabara sawa na kujenga vituo vitatu vya afya vya kata na kuweka vifaa tiba, tutunze barabara zetu”

 

 

Related Posts