Dkt. Samia Suluhu Hassan aweka jiwe la Msingi upanuzi na ukarabati wa Kiwanja cha Ndege cha Sumbawanga Mkoani Rukwa

RAIS Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aweka jiwe la Msingi upanuzi na ukarabati 

wa Kiwanja cha Ndege cha Sumbawanga Mkoani Rukwa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa kuashiria uzinduzi vihenge na maghala ya kisasa ya kuhifadhia nafaka ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi wa Chakula (NFRA), Kanondo, Sumbawanga Mkoani Rukwa tarehe 16 Julai, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi mara baada ya kuzindua vihenge na maghala ya kisasa ya kuhifadhia nafaka ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi wa Chakula (NFRA) Kanondo, Sumbawanga Mkoani Rukwa tarehe 16 Julai, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la Msingi ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi na Huduma (VETA) cha Mkoa wa Rukwa kilichopo Kata ya Momoka, Sumbawanga tarehe 16 Julai, 2024.
ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na viongozi mbalimbali, Wanafunzi na Wakufunzi wa Chuo cha Ualimu Sumbawanga Mkoani Rukwa tarehe 16 Julai, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akibonyeza kitufe kuashiria ununuzi wa nafaka kwa msimu wa 2024-2025 mara baada ya uzinduzi wa vihenge na maghala ya kisasa ya kuhifadhia Nafaka ya (NFRA), Kanondo, Sumbawanga Mkoani Rukwa katika muendelezo wa Ziara yake ya Kikazi mkoani rukwa tarehe 16 Julai, 2024.
Muonekano wa Kiwanja cha Ndege cha Sumbawanga ambacho ambacho kipo kwenye hatua mbalimbali za ujenzi kama inavyoonekana.

Vihenge na maghala ya kisasa ya kuhifadhia nafaka ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi wa Chakula (NFRA) yaliyopo Kanondo, Sumbawanga Mkoani Rukwa tarehe 16 Julai, 2024.

Related Posts