Klabu ya Azam FC imefanikiwa kuinasa saini ya kiungo mshambuliaji wa Kimataifa wa Mali, Cheickna Diakite mwenye umri wa mika 19 kutoka klabu ya Real Bamako.
Nyota huyo chipukizi (19), aliyepachikwa jina la staa wa Real Madrid Mbappe kutokana na kasi na uwezo wake wa kuipenya safu ya ulinzi ya timu pinzani, amesaini mkataba wa miaka mitatu utakaomfanya kudumu ndani viunga vya Azam Complex hadi mwaka 2027.