MBAPPE AFIKIA REKODI YA RONALDO MADRID – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

Nyota wa Real Madrid Kylian Mbappé, amefikia rekodi ya Cristiano Ronaldo ya kuwa na idadi kubwa zaidi ya Mashabiki waliojitokeza kwenye Sherehe za utambulisho wake kwenye Klabu hiyo huku akikusanya mashabiki 80,000.

 

 

Nyota huyo wa timu ya taifa Ufaransa alitambulishwa katika Uwanja wa nyumbani wa Real Madrid, Santiago Bernabeu na idadi ya Mashabiki waliojitokeza ili lingana na idadi ya Mashabiki walioudhuria utambulisho wa Cristiano Ronaldo mwaka 2009 kwa idadi ya Mashabiki 80,000.

 

 

Utambulisho wake umezipita takwimu za kihistoria za wachezaji kama Diego Maradona, ambaye watu 75,000 waliudhuria, Zlatan Ibrahimovic 60,000 na Neyma mashabiki 57,000.

 

 

Idadi hiyo inaonyesha ni jinsi gani Mbappe alivyo na ushawishi mkubwa kwenye soka huku Mashabiki wakionyesha mapenzi makubwa kwa nyota huyo.

Related Posts