BEKI wa Coastal Union ambaye pia inaelezwa kumalizana na Simba dirisha hili la usajili, Lameck Lawi anatajwa kutimka nchini hivi karibuni kwa ajili ya kujiunga na K.A.A Gent inayoshiriki Ligi Kuu Ubelgiji.
Lawi ambaye msimu ulioisha alionyesha uwezo mkubwa eneo la beki wa kati na kuisaidia timu yake kumaliza nafasi ya nne na kupata nafasi ya uwakilishi ligi Kombe la Shirikisho Afrika anatarajia kusafiri muda wowote kuanzia sasa.
KIUNGO wa zamani wa Simba, Said Ntibazonkiza ‘Saidoo’ anatajwa kujiunga na Rayon Sports ya Rwanda.
Saidoo aliyemaliza Ligi na mabao 11 akiwa kinara kwa upande wa Simba amekamilisha taratibu zote za kujiunga na miamba hiyo kilichobaki ni kusaini mkataba wa mwaka mmoja.
ALIYEKUWA kipa wa Dodoma Jiji, Aron Kalambo anatajwa kuwa kwenye hatua za mwisho kumalizana na Ken Gold kwaajili ya kuitumikia timu hiyo msimu ujao.
Kalambo ambaye ni zao la Tanzania Prisons amepita pia KMC ataungana na timu hiyo akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na Dodoma Jiji ambayo imempa mkono wa kwaheri.
KAGERA Sugar ipo kwenye hatua nzuri ya kukamilisha dili la kiungo mkabaji wa KCCA FC ya Uganda, Peter Lwasa.
Kwa mujibu wa taarifa zinaeleza kuwa mabosi wa Kagera Sugar wamempa kandarasi ya miaka miwili kiungo huyo.
COASTAL Union imeanza mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji wa Tabora United, Yohana Mkomola ambaye yupo huru baada ya mkataba wake kutamatika.
Nyota huyo wa zamani wa Yanga na Vorskla Poltava (Ukraine) inaelezwa kama mambo yatakwenda sawa anaweza kujiunga na wagosi wa kaya kwa mkataba wa mwaka mmoja.
WINGA wa zamani wa Mtibwa Sugar, Salum Kihimbwa inaelezwa yupo kwenye hatua za mwisho kusaini mkataba wa kuitumikia Singida Fountain Gate msimu ujao.
Mchezaji huyo ambaye amepita Dodoma Jiji, Tanzania Prisons na Mbeya City mazungumzo na Singida Fountaine Gate yamefikia katika hatu
CEASIAA Queens inayoshiriki Ligi kuu ya wanawake (WPL) inatajwa kuhitaji huduma ya beki wa kati wa Simba Queens, Silivia Mwacha anayemaliza mkataba klabuni hapo.
Inaelezwa Simba haitaendelea nae msimu ujao kutokana na ushindani wa namba aliokutana nao beki huyo, Fatuma Issa ‘Fetty Densa’ na Violeth Nicholaus.