JUKUMU LETU SOTE KUZINGATIA SHERIA KATIKA KUTOA NA KUPOKEA HUDUMA -MHE.SIMBACHAWENE

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene   akizungumza leo na wananchi wa Kijiji cha Maswala, Kata ya Pwaga iliyopo katika Jimbo la Kibakwe,  Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Jijini Dodoma, ikiwa ni mwendelezo wa  ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi  katika Jimbo hilo.

Sehemu ya wananchi wa Kitongoji cha Ng’onje kilichopo katika Kijiji cha Pwaga, Tarafa ya Kibakwe iliyopo katika Jimbo la Kibakwe, Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Jijini Dodoma wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene, wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika Jimbo la Kibakwe.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akisalimiana na baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Maswala mara baada ya kuwasili, ikiwa ni ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika Jimbo hilo.

Baadhi ya Waheshimiwa Madiwani wa Tarafa y ya Kibakwe iliyopo katika  Jimbo la Kibakwe, Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa jijini Dodoma wakitumbuiza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kuzungumza na wananchi hao ikiwa ni ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika Jimbo la Kibakwe.

Diwani wa Kata ya Kibakwe Mhe.Wilfred Mgonela  akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Ng’onje cha Kijiji cha Pwaga Kata ya Kibakwe iliyopo katika Jimbo la Kibakwe, Halmashauri ya  Wilaya ya Mpwapwa jijini Dodoma wakati wa ziara ya kikazi ya  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika Jimbo la Kibakwe.

Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, Mhe. Richard Maponda akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Maswala, Kata ya Kibakwe iliyopo katika Jimbo la Kibakwe, Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa jijini Dodoma wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika Jimbo la Kibakwe.

Na Mwandishi wetu – Kibakwe

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Mbunge wa Kibakwe, Mhe. George Simbachawene amewataka viongozi na wananchi kuzingatia Sheria za nchi katika kutoa na kupokea huduma.

Mhe. Simbachawene ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na wananchi kwa nyakati tofauti kwenye mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Maswala na Kitongoji cha Ng’onje vilivyopo Katika Kata ya Pwaga, Jimbo la Kibakwe, Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa jijini Dodoma, ikiwa ni mwendelezo wa katika Jimbo hilo.

Mhe. Simbachawene amesema ili kuendeleza amani na kuepusha machafuko basi sheria za nchi ni lazima zizingatiwe na kila mtu awe kiongozi au mwananchi wa kawaida.

Amesema Tanzania imejengwa kwa misingi ya haki na usawa na ndio maana rasilimali za nchi zinagawanywa kwa usawa katika maeneo yote ya nchi ili kuchagiza utawala bora na ndio maana imeendelea kuwa kisiwa cha amani.

Amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu ameendelea kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa kuzingatia utoaji wa haki na usawa kwa wananchi wote bila kujali mahali walipo.

Ameongeza kuwa katika Jimbo la Kibakwe analoliongoza miaka ya nyuma vijiji vingi havikuwa na huduma nyingi za kijamii ikiwemo shule na zahanati lakini kwa sasa huduma hizo zote zipo maeneo mengi na wananachi wanaendelea kuhudumiwa.

Katika hatua nyingine, Mhe. Simbachawene ametoa wito kwa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) pamoja na Wakala wa Umeme Vijijini (REA) kuhakikisha zinatoa kipaumbele cha huduma wanazozitoa kwa Taasisi za kijamii zilizopo katika Kata ya Pwaga.

Amesema huduma muhimu kama vile umeme na barabara ni muhimu zikafikishwa haraka katika maeneo ya shule, makanisa, misikiti pamoja na ofisi za vijiji.

Mhe.Simbachawene amesema Serikali imekuja na mpango mkakati wa ujazilizi ambapo vitongoji na maeneo yote ya pembezoni mwa miji itaanza kufikishiwa umeme.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Pwaga, Mhe. Wilfred Mgonela ametumia fursa hiyo kumshukuru Mhe. Simbachawene kwa ushirikiano ambao ameendelea kumpa katika kuhakikisha miradi ya maendeleo inaendelea kutekelezwa katika Kata anayoiongoza huku akiwaomba wananchi kuendelea kushirikiana naye ili kujiletea maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Kata kwa ujumla.

Related Posts