TIC yapongezwa kuweka mazingira mazuri na wezeshi kwa ajili ya kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Mipango na Uwekezaji Stanslaus Nyongo, ameeleza kuridhishwa na hatua kadhaa ambazo zimeendelea kuchukuliwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), katika kuweka mazingira mazuri na wezeshi kwa ajili ya Kuwavutia Wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.

Naibu Waziri Stanslaus Nyongo ametoa Kauli hiyo jana Julai 16, 2024 Jijini Dar es Salaam alipofika makao makuu ya ‘TIC’ ili kukagua utendaji kazi wa kituo hicho na kusikiliza Changamoto inazokikabili.

“Nimefika hapa kwa lengo la kuangalia namna Shughuli zinazofanyika hapa, kwa kweli nimeona na nimeridhishwa na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Uongozi wa TIC kwa kuweka mazingira mazuri na wezeshi kwa Wawekezaji mbalimbali wa ndani na Nje ya Tanzania” amesema.

Related Posts