DKT JAFO ARIDHISHWA NA UJENZI JENGO LA WMA, ATOA MAAGIZO KUFANYIKA UKAFUZI MITA ZA UMEME

Na Janeth Raphael MichuziTv

Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Suleiman Jafo ametoa Maagizo kwa Wakala wa vipimo Tanzania(WMA) kutembelea maeneo yote yanayotakiwa kufanywa ukaguzi hususani wa mita za umeme kabla hazijafika kwa mlaji ili kupima uthibiti wa mita hizo,kwa lengo la kuwapunguzia gharama wananchi na kuepuka kulipa gharama isiyo sahihi.

Dkt Jafo ameyasema hayo leo Jijini Dodoma July 17,2023 mara alipofanya ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi unaoendelea wa jengo la ofisi za Wakala wa Vipimo Tanzania.

Na kuongeza kuwa ameridhishwa na kasi iliyopo katika ujenzi huo pia gharama na fedha zilizowekezwa katika ujenzi huo zinaridhisha.

“Kikubwa niitake Taasisi hii iendelee kufanya kazi yake kwa Weledi kama inavyofanya siku zote, Lakini nawataka waende wakague maeneo yote ambayo yanatakiwa yafanywe ukaguzi hususani ni katika mita za umeme kabla hazijaenda kwa walaji lazima zifikishwe kwa Wakala wa vipimo kuweza kuangalia uthibiti wa mita hizo kwa lengo la kuwapunguzia gharama wananchi wa kufunga mita ambayo haina ubora na mwisho wa siku kulipa bili isiyo sahihi”.

“Nikiwa kama Waiziri nimeridhishwa sana na thamani ya fedha na hasa uje zi wake unavyoenda lakini vilevile kasi kazi imenifurahisha maana yake nikiangali mpaka mwezi Januari na hali ilipofikia nina matumaini litakamilika hata kabla ya muda uliopangwa”.

Aidha Dkt Jafo amesema pamaoja na Wakandarasi kuendelea kufanya kufanya vizuri ila wahakikishe unakamilika ndani ya muda na hata ikiwezekana kabla ya muda ili kuweza kuondoka katika maeneo ya kupanga ili kupunguza baadhi ya gharama ambazo zimekuwa zikitumika katika kulipa kodi.

“Kwahiyo niwatake Wakandarasi hawa hata kama wanaendelea vizuri,wahakikishe ujenzi huu unakamilika ndani ya muda hata ikiwezekana kabla ya muda wa Januari jengo hili liweze kukamilika . Lengo kubwa tuweze kuhama katika maeneo ya kupanga tuje katika jengo letu wenyewe, kwasababubkuoanga tunatumia kodi ambapo tukija katika jengo letu tunakuwa tumepunguza gharama zingine “.

Mbali na hayo yote Waziri hakuacha kuwapongeza Wataalam wa Wakala wa vipimo Tanzania kwa kutumia mapato ya ndani kujenga jengo hilo, kwani hii inaashiria kuwa hii ni miongoni mwa Taasisi zinazofanya vizuri.

Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa vipimo Tanzania Bwana Joseph V Maliti amesema kuwa ujenzi wa jengo hili unagaharimu kiasi cha Shiling Bilioni 6, na mpaka sasa ujenzi umefikia asilimia 81.5 na kazi nyingi zilizobaki mpaka sasa ni za nje ikiwemo Mashimo ya kuhifadhia maji taka.

“Ujenzi wa jengo hili unagharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 6 na Mpaka sasa ujenzi umefikia asilimia 81.5 na kwa upande wa kazi zilizobaki nyingi ni za nje ikiwemo ujenzi wa mashimo ya kuhifadhia maji taka”.

Naye Mhandisi Justin Kyando ambaye ni Mhandisi wa Kampuni ya Ujenzi ya Mohammed Builders amesema kuwa kazi zilizosalia ni chache ukilinganisha muda uliobaki ambapo wanatakiwa kukabidgi kazi Januari 2025 hivyo watahakikisha kila kitu kinakwenda vizuri na kwa wakati.

Hii ni Ziara ya Waziri Jafo ya ukaguzi wa maeneo mbalimbali yanayohusu Wizara ya Viwanda yenye lengo ya Taasisi zote zilizo chini ya Wizara ziweze kufanya kazi zake kutoka makao makuu.

Ujenzi wa jengo hili la Wakala wa vipimo Tanzania umegharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 6, na uanatarajiwa kukamilika Januari 2025.



Related Posts