SHINDANO la Mtindo wa Maisha (Life style) Kwa Vijana wenye ushawishi Mitandaoni ( BINGWA ) Msimu wa tatu umezundiliwa rasmi Vijana Mikoani wapewa nafasi .
Akizungumza na Wanahabari Leo Aprili 24,024 Ukumbi wa Serena Hoteli Jijini Dar es Salaam wakati wa kuzindua Shindano hilo kwa Msimu wa tatu Meneja wa Shindano hilo Ombeni Phiri amesema Shindano hilo limewapa fursa Vijana wengi mitandaoni kubadilisha maisha kutokana na fursa mbalimbali ambazo wamekuwa wakizipata na hivyo kulazimika Shindano hilo kuendelea kuwepo ambapo msimu huo wa tatu umekuwa wa kitofauti zaidi.
“Misimu miwili imekuwa yenye Mafanikio makubwa zaidi na Vijana wengi wa mitandao kuonesha Maisha yao halisi wanapokuwa kwenye mjengo huo hivyo kwa Msimu huu watatu Umepewa nguvu na Kampuni ya Kubashiri ya Parimatch ili kumsukuma Mshindi huyo kufanya vitu vikubwa zaidi Pape Shindano linapomalizika
Msimu Mpya wa tatu wa show ya Bingwa itatembelea Mikoa mitano kwa ajili ya kutafuta Vijana wengine ambapo maoni mengi yamekuwa yakiwafikia Vijana wakihitaji kushiriki Shindano hilo.
“Msimu wa tatu umefanya Maboresho mbalimbali ikiwemo ongezeko la Mikoa mitano ya washiriki ikiwemo Arusha, Dodoma,Mwanza, Mbeya pamoja na kitovu chenyewe Dar es Salaam.
Pia ameeleza kuwa usahili kila Mkoa utachukua washiriki 10 kila Mkoa na kufatia mchujo katika App ya Startimes (Startimes On) ambapo washiriki 08 watatoka Dar hivyo kukamilisha Jumla ya watakaoingia ndani ya nyumba washiriki 24 huku zawadi ya Mshindi kugharimu zaidi ya Milioni 35 za Kitanzania.
Kwa Upande wake Meneja Masoko wa Kampuni ya Startimes David Malisa amesema Msimu wa tatu utaendelea kuwapa fursa vijana zaidi na Atakaeibuka Mshindi Kampuni ya Startimes itaweza kumpa Ubalozi.
Aidha amewapongeza Kampuni ya Parimatch kuona haja ya kuwapa Moyo Vijana hao wenye ushawishi Mitandaoni kukuza vipaji vyao.
Pia amewataka wateja kulipia vifurushi cha Uhuru elfu 23000 ili kuweza kuona shindano hilo kupitia Tv3 ndani ya King’amuzi cha Startimes.
Nae Meneja Masoko wa Parimatch Levis Paul ameeleza sababu ya Kampuni hiyo kuishika mkono Shindano hilo la ” Bingwa”.
“Sababu ya Parimatch kuungana na Msimu wa tatu wa Shindano la bingwa ni kutokana na shindano hilo Kuhusisha Vijana na Kauli mbiu ikibeba Jumba la Washindi ambapo Kampuni yetu inalenga zaidi kutafuta Washindi walipo kwa kupitia ubashiri.”
Paul ameeleza wao kama Parimatch wanatambua kuwa Washiriki wanahitaji kukaa siku 70 ambapo kila kitu kinahitaji uwezeshwaji kuanzia Malazi na vitu mbalimbali hivyo Tv3 na Startimes peke wanahitaji nguvu ya ziada ya kuendesha Shindano hilo hivyo sisi tumeona tuongeze nguvu hiyo kwa msimu huu wa tatu.”
Pia amefafanua zaidi kuwa Wana amini kuwa chapa ya Kampuni hiyo ipo sehemu na sahihi hivyo kudhamini shindano hilo itaongeza na kujiweka kwenye nafasi nyingine nzuri zaidi ya kujitangaza kama Kampuni.
Meneja programu wa shindano la Bingwa Ombeni Phiri akieleza namna Shindano hilo litakavyoshirikisha Mikoa mitano ambayo ni Arusha,Mbeya,Mwanza,Dodoma pamoja na Dar es Salaam
Meneja Masoko wa Kampuni ya Startimes David Malisa akizungumza na Wanahabari Leo Aprili 24,2024 Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam wakati wa Uzinduzi wa Msimu wa tatu wa Shindano la Bingwa ambapo amewataka wateja wa Kisimbuzi cha Startimes kulipia kifurushi ili kuendelea kuona shindano hilo kupitia Tv3
Meneja Masoko wa Kampuni ya Parimatch Levis Paul akizungumza machache mara baada ya Kuzinduliwa kwa Msimu wa tatu wa Shindano la Bingwa ambapo msimu huo Kampuni hiyo ikiwa wadhamini wakuu wa shindano