Waziri huyo amesema matokeo ya uchaguzi hayawezi kuamuliwa na kile kinachowekwa kwenye sanduku la kura pekee akisema kuna mbinu nyingine zinazoweza kumfanya mgombea kushinda.
Kiongozi wa chama cha wananchi CUF, Mohammed Ngulangwa mbali ya kuikosoa kauli hiyo lakini pia amesema ni kauli yenye kuudhi na kuleta ukakasisi katika taifa ambalo linajinadi kuimarisha demokrasia na kuzingatia utawala wa sheria.
Kauli hiyo imeibua hisia kali kutoka kwa makundi mbalimbali hasa wakati huu ambao taifa hilo likijiandaa kuelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa.
Waziri huyo alinukuliwa akisema matokeo ya uchaguzi hayawezi kuamuliwa na kile kinachowekwa kwenye sanduku la kura pekee akisema kuna mbinu nyingine zinazoweza kumfanya mgombea kushinda.
CCM yajiweka kando na matamshi ya Nape
Chama chake tawala CCM, kimetangaza kujiweka kando na kauli Nape na kwamba chama hicho hakiamini kushinda uchaguzi kwa mazingira ya utatanishi. Waziri Nape aliomba radhi kwa kauli hiyo.
Wachambuzi wa mambo wanaonya kuhusu kuendelea kuwaacha wanasiasa kutoa kauli zinazoweza kuwavunja moyo wapiga kura hasa kwa kuzingatia yale yaliyojitokeza katika uchaguzi uliopita wa mwaka 2019 wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 unaodaiwa kuchakachuliwa matokeo yake.
CCM yawaonya makada wake kuelekea mbio za uchaguzi
Chama chake tawala CCM, kimetangaza kujiweka kando na kauli hiyo ya mwanasiasa wake. Katibu wa uenezi na itikadi wa chama hicho, Amos Makalla amesema CCM haimani kushinda uchaguzi kwa mazingira ya kimezengwe zengwe.
Tayari mwenyewe Nape amejitokeza hadharani na kuomba radhi kuhusiana na kauli yake hiyo akisema aliifanya kwa masihara tu.