WANANCHI WAMLAZIMISHA MBUNGE KUNYWA MAJI MACHAFU

 

Na Nasra Ismail
Wananchi wa Kijiji cha Mwamboku Kata ya Kashishi ,wamelazimika kumpelekea Mbunge wa Jimbo la Msalala Iddi Kassim Iddi maji ambayo wanatumia kwa sasa huku wakimuomba kushughulikia tatizo la upatikanaji wa maji kwenye kijiji chao kwani maji wanayotumia  wanatumia pamoja na mifugo.
Wananchi hao wamefikisha kilio chao kwenye mkutano wa hadhara ambao umeitishwa na Mbunge wa Jimbo hilo ,ambaye alifika kwa lengo la kusikiliza kero mbalimbali ambazo zinawakabili wananchi.
Wamesema kukosekana kwa maji safi na salama katika kijiji chao kimekuwa ni tatizo kubwa ambalo linapelekea kuchangia maji na mifugo na kwamba ni vyema kwa Mbunge akabeba kilio chao na kukisemea waweze kupata maji safi.
“Mbunge wetu tunatambua wewe ni mchapakazi na kazi zako tunaziona kinachotusikitisha na leo tumeona tukulete maji tunayotumia tuone kama unaweza kuyatumia sisi hapa kilio chetu kikubwa ni maji tu ukitusaidia maji yakapatikana tunasema kutoka moyoni  utakuwa umetusaidia sana” Alisema Diana Dalali Mwananchi wa Mwamboku.
Kufuatia kilio cha wananchi imemlazimu Mbunge  Iddi kumpigia simu Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kahama kujua ni lini wataanza kusambaza maji kwenye kijiji hicho,ambapo Meneja amesema wanafuatilia kuomba msamaha kwenye kodi ya Bomba ndani ya wiki mbili zitakuwa zimefika na kuanza kusambaza maji.
“Ndugu zangu wananchi niwaondoe wasi wasi kuhusu upatikanaji wa maji mmemsikia meneja amesema ndani ya wiki mbili bomba zitaanza kuchimbwa na kupelekwa maji kwa wananchi naombeni mnisamehe sana wakati mwingine mimi Mbunge nikitoa maagizo ni wajibu wa diwani na mwenyekiti kufuatilia kujua hatua ambazo zimefika na kama wanakwamba wanarudi kwangu”Iddi Kassim Iddi Mbunge Jimbo la Msalala.

 

Related Posts