Makubaliano ya kuweka chini silaha DRC yarefushwa siku 15 – DW – 18.07.2024

Msemaji wa Baraza la Kitaifa la Usalama la Ikulu ya Marekani, Adrienne Watson amesema wamejitolea kufanya kazi na serikali za DRC, Rwanda, na Angola kutumia nyongeza hiyo ya kuweka chini silahakatika kubainisha mfululizo wa hatua za kufikia usitishaji wa kudumu wa uhasama.

Jimbo la Kivu Kaskazini limekabiliwa na mapambano ya waasi wa M23 zaidi ya miaka miwili pamoja na vurugu za makundi mengine ya wenye kujihami kwa silaha.

Marejeo ya shutuma za kimataifa kwa Rwanda kuhusu DRC

Kambi ya wakimbizi ya Goma DR Congo
Wakazi wakitazama onyesho la mitindo lililofanywa na warsha ya ndani iitwayo Kuliko Art katika kambi ya wakimbizi nje kidogo ya Goma, kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, Aprili 15, 2022.Picha: Zanem Nety Zaidi/Xinhua/IMAGO

Kongo, Umoja wa Mataifa na mataifa ya Magharibi mara kwa mara zimekuwa zikiishutumu Rwanda kwa kuunga mkono M23 kwa kuwatumia wanajeshi wake na silaha, madai ambayo imekuwa ikiyakanusha.

Kwa upande wake Rwanda inaishutumu Kongo kwa kufadhili na kupigana bega kwa bega na Kundi la waasi wa Kihutu la FDLR, ambalo linaelezwa kuishambulia jamii ya Kitutsi katika nchi zote mbili.

Soma zaidi:Waasi wa M23 waendelea kukamata miji muhimu ya Kongo

Kwa upande wake kundi la M23 lliasema linapigania kuwalinda Watutsi dhidi ya wapinzani kama FDLR, ambao wamajumuisha jamii ya Wahutu yenye msimamo mkali waliokimbiliaKongo baada ya kushiriki katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 yaliyolenga Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa wastani nchini Rwanda.

Chanzo RTR

 

Related Posts