BI FATMA KARUME AMJIA JUU MZEE MAGOMA – MWANAHARAKATI MZALENDO

Kwenye kipindi cha #JahaziHD kinachorushwa na kituo cha Clouds FM, Bi Fatma amevunja ukimya na kueleza msimamo wake kwa kile ambacho kimekua kinazungumzwa kuwa ni moja ya watu waliosaini kufunguliwa kwa Kesi inayoihusu klabu ya  Yanga SC

 

 

“Huyo Mzee Magoma kwanza simjui, wala hakuja mtu kwangu kuniambia jambo lolote. Inanishangaza mahakama kutoa hukumu bila sisi wahusika wanaotajwa kwenye kesi kupewa taarifa. Wameniudhi sana hao waliopeleka jina langu kwenye hiyo kesi.

 

 

“Sitakubali, wamenidharau wameniabisha kwa kutumia sahihi yangu. Kwanini mahakama haikunitafuta kuniuliza kama kweli nimewapa ruhusu ya kutumia sahihi yangu? Nitawachukulia Sheria kwani wamenitukana hadharani” amesema Bi Fatma Karume

 

Related Posts