Tume ya haki za binadamu yafuatilia haki ya wafanyakazi kwenye kilimo Njombe “Lengo uwekezaji usiwe na madhara kwa binadamu”

Ili kulinda na kuhakikisha shughuli za uwekezaji zinaendelea bila kuwa na madhara kwa binadamu,tume ya haki za binadamu chini wizara ya katiba na sheria imefika na kufuatilia namna wawekezaji kwenye sekta ya kilimo mkoani Njombe wanavyo jali sera ya haki za binadamu kwenye maeneo yao ya uwekezaji.

Dkt.Thomas Masanja ni kamishna wa tume ya haki za binadamu na utawala bora akizungumza na waandishi wa habari mkoani Njombe amesema wamefika katika mkoa huo kwa lengo la kufuatilia na kukusanya taarifa juu ya uandaji wa hali halisi ya haki za binadamu ili kusaidia mpango kazi wa kitaifa kuhusu haki za binadamu na biashara.

“Mpango kai huu ni kwa ajili ya kuratibu shughuli za uwekezaji nchini na mambo ya haki za binadamu ili zisiwe na athari mbaya kwa watu kwa maana ya haki zao”amesema Masanja.

Amesema kwa mkoa wa Njombe Tume ya haki za binadamu imejikita zaidi na uwekezaji kwenye sekta ya kilimo ili kuona kwa sasa kabla mpango kazi haujaandaliwa ni kwa namna gani wawekezaji wamekuwa wakijali haki za binadamu ambapo miongoni mwa maeneo yanayopitiwa ni katika kiwanda cha chai Kibena pamoja na jamii inayozunguka mashamba hayo.

Kwa upande wake katibu tawala wa mkoa wa Njombe Judica Omary amesema wakazi wa mkoa wa Njombe kwa kiasi kikubwa wanajihusisha na kilimo huku kilimo huku sekta ya Chai ikiwa ni moja ya sekta yenye uwekezaji mkubwa hivyo tume ya haki za binadamu kwenda kufanya kazi katika eneo hilo kutaenda kusaidia na kukumbusha uzingatiaji wa haki za binadamu katika sekta hiyo.

“Kwa kuzingatia sheria na kanuni hilo ni eneo mojawapo ambalo wanakwenda kuangali kama haki inatendeka wataangalia kama sheria na taratibu zilizowekwa je zinatekelezwa ipasavyo kwa hiyo wataangali haki zote ikiwemo ulipaji wa watumishi,staha,afya ya mfanyakazi na mambo mengine”amesema Judica

Vile vile amesema mkoa wa Njombe unatoa ushirikiano kwenye kila linalohitajika ili kusaidia kuandaa mpango utakaoweza kuwa na manufaa kwa watanzania na wananchi wa mkoa wa Njombe.

Related Posts