Geita Gold yaaanza na kocha

GEITA Gold imeanza kujipanga kusajili kwa ajili ya Ligi ya Championship, imemsajili kocha Aman Josiah kwa mkataba wa mwaka mmoja, ili kuipandisha timu hiyo msimu ujao.

Kocha huyo, msimu ulioisha alikuwa na Biashara United, ambayo ilishindwa kupanda Ligi Kuu Bara baada ya kucheza mtoano na Tabora United iliyowafunga jumla ya mabao 3-0, hivyo ikamaliza nafasi ya nne kwenye msimamo.

Kutokana na mchango wake Biashara, uongozi wa Geita Gold umeona ana uwezo mkubwa wa kuisaidia timu hiyo kupanda.

Kiongozi wa Geita ambaye hakutaka kutajwa jina lake, alisema “Baada ya timu kushuka daraja,kumefanyika mabadiliko makubwa, ikiwemo baadhi ya wachezaji wao kupata timu za Ligi Kuu, makocha kuondoka, hivyo ni kama wanatengeneza timu upya.

Aliongeza”Pia tunazingatia uimara wa ligi ya Championship, ndio maana tunasajili kocha mzuri pia tunatafuta wachezaji wazuri, naamini msimu ujao tunaweza kurejea tena Ligi Kuu.

Related Posts