KUELEKEA msimu ujao Yanga Princess imekamilisha usajili wa kiungo Agness Pallangyo kutoka Fountain Gate Princess.
Inaelezwa Yanga baada ya kukwama kwenye dili la kiungo wa JKT Queens, Amina Bilal ikamuibukia Agnes ambaye amemaliza mkataba wake kikosini.
Chanzo kimeiambia Mwanaspoti kuwa mchezaji huyo amepewa mkataba wa miaka miwili kukitumikia kikosi hicho.
“Ni mchezaji mzuri na kwa Yanga anaweza kuwasaidia kama ataendelea na kiwango chake tayari amesaini mkataba na kilichobaki ni wenyewe kumtambulisha,” kimesema chanzo hicho.
Takribani wachezaji 12 wa Fountain Gate Princess wanaripotiwa kuondoka kutokana na kile kinachodaiwa kuwa changamoto ya kifedha.