Dar es Salaam. Wakati mjadala wa mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yaliyowaondoa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, January Makamba na aliyekuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Rais Samia Suluhu Hassan amefanya utenguzi wa viongozi wa taasisi za mawasiliano nchini.
Katika taarifa kwa umma iliyotolewa leo Jumanne Julai 23 2024 na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, Rais Samia ameligusa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Shirika la Posta na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF).
Waliotenguliwa ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TTCL Zuhura Muro na Mkurugenzi wa shirika hilo, Peter Ulanga na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta Tanzania Brigedia Jenerali mstaafu Yohana Mabongo.
Wengine ni Postamasta Mkuu, Shirika la Posta Tanzania Maharage Chande, Profesa John Nkoma ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya UCSAF na Ofisa Mtendaji Mkuu wake, Justina Mashiba.
Endelea kufuatilia Mwananchi.