AYOUB LAKRED NJE YA UWANJA MIEZI SITA – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

Kipa namba moja wa Simba SC, Ayoub Lakred anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa miezi sita baada ya kuumia katika kambi ya timu hiyo nchini Misri.

 

Ayoub raia wa Morocco amepata majeraha ya nyama za Paja zitakazomuweka nje kwa kipindi hicho.

 

 

Kitendo cha Ayoub kuumia kunafanya Simba SC ibakiwe na makipa wawili ndani ya kambi hiyo ambao ni Ally Salim na Hussein Abel, huku uongozi ukitajwa kuwa mbioni kumuwahisha nchini humo Aishi Manula ambaye hakuwa sehemu ya kambi.

Related Posts