NOVATUS DISMAS AJIUNGA NA KLABU HII – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

Kiungo Mtanzania Novatus Dismas Miroshi mwenye umri wa miaka 21 amejiunga na Club ya Goztepe ya Uturuki kwa mkataba wa miaka minne baada ya kumaliza mkataba wake wa mkopo Shakhtar Donetsk ya Ukraine.

 

 

Novatus msimu uliopita alicheza Shakhtar aliyojiunga nao akitokea Zulte Waregem ya Ubelgiji kwa mkopo wenye kipengele cha kununuliwa moja kwa moja lakini hilo halikufanikiwa.

 

 

Goztepe ni timu iliyopanda kucheza Ligi Kuu Uturuki msimu wa 2024/2025 baada ya kumaliza nafasi ya pili msimu uliopita katika Ligi daraja la kwanza Uturuki.

Related Posts