Mkakati mkubwa wa teknolojia ya kifedha, kuimarisha uwezo wa biashara za wasambazaji wa ndani na wajasiriamali wazinduliwa

Katika mkakati unaolenga kuleta mabadiliko kwenye sekta ya biashara, na kuendeleza upatikanaji wa huduma za kifedha nchini Tanzania kwa ufanisi zaidi benki ya Stanbic Tanzania inashirikiana na Ramani, kampuni namba moja kwenye teknolojia ya kifedha, malengo yakiwa kutumia teknolojia na msaada kubwa ya kifedha, kuimarisha uwezo wa biashara za wasambazaji wa ndani na wajasiriamali.

Muunganiko huu unalenga kutumia miundombinu ya kifedha ya kisasa ya Ramani, pamoja na rasilimali imara za kifedha za Benki ya Stanbic. Pia, utasaidia zaidi ya wasambazaji 100 katika mwaka wake wa kwanza, ukiangazia mnyororo muhimu wa thamani katika sekta ya Bidhaa za Watumiaji (FMCG).

Pamoja na majukwaa ya teknolojia ya hali ya juu na mikakati ya kifedha, ushirikiano huu utakabiliana na vipengele muhimu vya usimamizi wa biashara, ufuatiliaji wa mauzo, na miamala ya kidijitali ili kuongeza ufanisi wa uendeshaji kwa wasambazaji.

Fredrick Max, mkuu wa kitengo cha biashara wa Benki ya Stanbic Tanzania, alisema, “Ushirikiano wetu na Ramani ni zaidi ya biashara; ni ushirikiano wa kimkakati ambao unaahidi kubadilisha jinsi biashara inavyofanywa nchini Tanzania. Kwa kuunganisha nguvu zetu na maono yetu, tunapanga kusaidia mahitaji ya kifedha ya wasambazaji wa ndani, na pia kuchangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa uchumi wa taifa letu.”

Lengo kuu ni kutoa fedha kwa wasambazaji na wauzaji, ili kuboresha usimamizi wa ugavi kwa wasambazaji, na wafanyabiashara wa bidhaa kubwa .

Hii itawezesha usimamizi bora wa manunuzi, udhibiti wa hisa, na ufuatiliaji wa mauzo ya kidijitali, katika kuimarisha michakato ya biashara na miamala ya kifedha.

Related Posts