ATOLEWA UVIMBE KILO 1.4 KATIKA KIZAZI, ALIISHI NAO MIAKA MITANO – MWANAHARAKATI MZALENDO

 

MAMA wa watoto wanne, mkazi wa Siha, mkoani Kilimanjaro (jina tunalo), ametolewa uvimbe wenye uzito wa kilogramu 1.4 katika kizazi ambao ameishi nao kwa zaidi ya miaka mitano.

 

Uvimbe huo kitaalamu unaitwa ‘mayoma’ ulikuwa unaendelea kuota katika kizazi, huku ikielezwa ulikuwa na uwezekano wa kutokea ndani ya mfuko wa uzazi au pembeni mwa ukuta wa kizazi.

 

Akizungumzia upasuaji huo uliofanywa na jopo la madaktari bingwa wa magonjwa ya wanawake, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Siha (DMO), Dk. Paschal Mbotta, alisema upasuaji huo uliochukua saa mbili na nusu, ulilenga zaidi kumwepusha mama huyo (44) na maumivu makali aliyokuwa akiyapata pamoja na kumwepusha kupata saratani ya kizazi.

 

“Tulikuwa na kambi ya siku tano ya madaktari bingwa wa magonjwa ya wanawake, ambayo tuliifanya kwa kutumia mapato ya ndani ya hospitali yetu ya Wilaya ya Siha.

 

Related Posts